Jumanne , 19th Apr , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la kigamboni hii leo, kuanzia saa mbili asubuhi.

Muonekano wa Daraja la Kigamboni

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewataka wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya kutumia daraja hilo itafungwa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nane mchana ili kuwezesha kufanyika kwa hafla ya ufunguzi.

Aidha huduma katika daraja la kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa nane mchana mara baada ya Mheshimiwa Rais kufungua daraja hilo rasmi.

Daraja la Kigamboni lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa Kilometa 2.5. ambapo Ujenzi wa daraja hilo umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.