Magufuli amkabidhi nyumba Mwinyi,akagua ya Kikwete

Jumapili , 18th Oct , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, amewataka wakandarasi kuharakisha ujenzi wa nyumba ya Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete.

Rais Mstaafu mwinyi na Mkewe wakiwa wameshikilia mfano wa funguo baada ya kukabidhiwa na Rais John Pombe Magufuli nyumba waliyojengewa kwa mujibu wa sheria.

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba, 18,2020 jijini Dar es salaam, wakati akikabidhi nyumba kwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi, ambapo pia amefanya ukaguzi wa nyumba ya Dkt.Jakaya Kikwete, na kudai kuwa nyumba hizo si zawadi bali zimejengwa kwa mujibu wa sheria.

       Kushoto ni Rais mstaafu awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Kulia ni Rais Dkt. John Pombe           Magufuli

''Kama hamuwezi wapeni JKT kazi ya ''Ucontractor'' fanyeni kazi ikamilike mimi sasa nitakua nakuja siku nikiwa napitapita barabarani siku nyingine nitakua napita hapa tumeshakubaliana kabla 31 Januari'' amesema Dkt.John Magufuli

Aidha Rais Magufuli amemtaka mkandarasi kuongeza wafanyakazi kazi katika mgawanyo wa majukumu ili kukamilisha ujenzi huo.