Rais Dk Mwinyi azidi kuwaamini ACT Zanzibar 

Jumatano , 3rd Mar , 2021

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, amewateua wanachama wawili wa Chama cha ACT-Wazalendo, Omar Said Shaaban na Nassor Ahmed Mazrui kuwa mawaziri. 

Kushoto ni Omar Said Shaaban, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda na kulia ni Nassor Mazrui, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Afya

Uteuzi huo umeanza hii leo Machi 3, 2021, ambapo Omar Shaaban, ameteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda huku Nassor Mazrui, ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

Mwingine aliyeteuliwa leo ni Dkt. Saada Mkuya Salum, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na wote kwa pamoja wataapishwa kesho Machi 4.