Queen Sendiga, Mkuu wa mkoa wa Iringa mteule
Taarifa ya uteuzi wa viongozi hao imetolewa hii leo Mei 15, 2021, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambapo miongoni mwa walioteuliwa ni Ali Hapi kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Anthony Mtaka kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma, David Kafulila kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.
Wengine ni Aboubakar Kunenge kuwa mkuu wa mkoa wa Pwani, Meja Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti kuwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Stephen Kagaigai kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Albert Chalamila, kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Juma Homera kuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya.
Tazama orodha ya wakuu wa mikoa mingine hapa chini