Jumatatu , 23rd Jun , 2014

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa tamko la kuanza kwa operesheni maalum nchi nzima ya kuwashurutisha waendesha pikipiki, baiskeli na maguta kuzingatia sheria za barabarani kutokana na kukiuka sheria za barabarani na kusababisha ajali.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania, Advera Senso.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania SSP Advera Senso wakati akiongea na vyombo vya habari.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Nchini limeeleza pia kuanza operesheni maalum ya kuzuia ngoma maarufu kwa jina la kigodoro katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kuonekana kukiuka maadili.