Jumatatu , 4th Jul , 2022

Watu sita wa familia moja wakazi wa kitongoji cha Kakonkwe kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma Mkoa wa Kigoma, wameuawa na watu wasiojulikana  kwa kuwapiga na kitu chenye ncha kali vichwani na mwilini na kumjeruhi mtoto wa miaka minne na kumwacha hai mtoto mwingine wa miezi mitatu.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Nasib Mpozemenya wamesema tukio hilo limeacha simanzi kijijini hapo.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi wa polisi Menrad Singano  amesema polisi imeanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa huku mkuu wa wilaya ya Kigoma Esther Mahawe akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola.