Jumanne , 10th Mar , 2015

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma PAC imemtaka Msajili wa Hazina nchini kuharakisha Mchakato wa kuanzishwa kwa Shirika jipya la Ndege.

Akitoa Maagizo hayo leo jijin Dar es salaam Mwenyekiti wa PAC mh. Zito kabwe amesema mpk tarehe30 june Msajili wa hazina apeleke ripoti ya Agizo hilo huku akiwataka kuyatumia mashiriki kama TANAPA na Ngorongoro Kama wana hisa katika shirika hilo jipya la Ndege,

Kwa Upande wake Msajili wa hazina Lawrence mafuru amesema atajitahidi kuratibu zoezi hilo ambalo lilianza toka mwaka2012 bila mafanikio yoyote,

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege la Taifa Salim Msoma amesema ni wakati wa Wawekezaji wa ndani kununua Hisa katika Mashirika ya Umma ili kujiepusha na wawekezaji wababaishaji toka nje huku tukiwa na wadau wa ndan wenye uwezo wa kuwekeza na wenye uzalendo