Jumanne , 10th Mar , 2015

MKUU wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi wamewataka wadau wa ukuzaji na uendelezaji wa maziwa kuhakikisha wafugaji wa mkoa wa Njombe hasa wanawake wanakuwa wazalishaji wakubwa wa maziwa na kuhakikisha mkoa wa Njombe unakuwa kinala wa uzalishaji.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi.

Akizungumza katika maadhinisho ya siku Wanawake ambapo kwa mkoa wa Njombe yamefanyika katika kijiji cha Lole Kata ya Ikuna halmashauri ya Njombe, na maandalizi yake kufanywa na shirika la ukuzazi wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (East Africa Dairy Development, EADD), ameutaka mradi kuhakikisha inakuza wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa na ifikapo mwisho wa mwaka huu yanakuwa yamesambaa nchi nzima.

Nchimbi amesema kuwa katika ukuzaji wa wafugaji wahakikishe wanawake ndio wanakuwa vinala katika ukuzaji wa uzalishaji wa maziwa na kwa kuwa mkoa wa Njombe kunakuja uwekezaji mkubwa wa uchimbaji wa madini ya chuma na makaa yam awe wahakikishe wanawezesha mkoa wa Njombe kuwa ndio unalisha wawekezaji katika machimbo hayo.

Amesema kuwa kufikia mwisho wa mwaka huu mradi huo uwe umeweza kukuza wafugaji na maziwa ya kutoka mkoani hapa yanakuwa yamesambaa nchi nzima na kuwa sio kwamba maziwa kutoka sehemu nyingine yasimame bali maziwa ya mkoa wa Njombe kwa kuwa yanapenda hivto wahakijishe maziwa haya yanafika kila kona mikoa ya hapa nchini.

Naye mkurugenzi mkazi wa mradi EADD, Mack Tsoxo, amesema kuwa mradi huo unao lenga mikoa ya nyanda za juu kusini ya Mbeya, Iringa na Njombe kwa tanza nia ni mradia ambao pia upo katika nchi za Uganda, Kenya na Ruanda umelenga kuinua wafugaji kw akupata kipato kupitia maziwa na marisho.

Amesema kuwa wananchi wa mikoa wa nyanda za juu watapatiwa uwezeshwaji wa kuboreshewa afya za mifugo yao, kutafutiwa masoko ya uhakika na kuhakikisha mifigo yao inakuwa yenye manufaa kwao kwa kuboresha ,maisha kutokana na mazoa ya maziwa.

Aidha baadhi ya wafugaji walio nufakika na kupitia mradhi huo wameelezea hisia zao na kuwa wamefufaika kuzalisha maziwa mengi zaidi baada ya kuingia kwa mradi huo na sasa nameweza kuwa na kipato cha kutosha kutokana na maziwa na uzalishaji wa marisho.