Jumanne , 8th Dec , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imetanga uchaguzi wa majimbo ya Arusha mjini na Handeni Mjini mkoani Tanga utafanyika tarehe 13 Desemba, baada ya kuahirishwa kufuatia kufariki kwa wagombea ubunge katika majimbo hayo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi huu ni zilezile zilizotumika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Amesema mara baada ya kupiga kura na kwa kuzingatia maadili ya uchaguzi ya 2015 yaliyokubaliwa na vyama vyote vya siasa nchini vilivyoingia kwenye uchaguzi mkuu na kuridhiwa na mahakama, wapiga kura wanatakiwa kuondoka vituoni na kuendelea na shughuli zao.

Wakati huo huo Jaji Lubuva amesema amepokea tatizo la baadhi ya maafisa wa NEC kutolipwa stahiki zao baada ya uchguzi kuisha hivyo atalifwtilia na atahakikishamaafisa hao wanalipwa stahiki zao bila pungufu yeyete..