Ijumaa , 13th Jan , 2017

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imevitaka vyama vya siasa vilivyo simamisha wagombea katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani kuzingatia taratibu na kutumia haki yao ya kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa maadili.

Kailima Ramadhani

Imesema vyma hivyo vinapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwenye ngazi husika kabla ya masaa 74 ili malalamiko yoa yashugulikiwe kwa wakati.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusiana na malalamiko yaliyotolewa na chama cha ACT Wazalendo hapo jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana Ramadhani Kailima amesema bado chama hicho kina nafasi ya kuwasilisha malalamiko yao katika ngazi zote hadi pale watakapoona wameridhishwa na hatua zilizochukuliwa.

Aidha, Bwana Kailima amewataka wananchi kutompatia mtu yeyote kadi yake ya kupiga kura isipokuwa kuionyesha katika kituo cha kupiga kura siku ya kupiga kura na kuwaonya wale wote wanaomiliki kadi ya mpiga kura isiyokuwa yake kinyume cha sheria.

Mbali na suala hilo Bwana Kailima amewataka wagombea wa vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu na kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi.