Jumanne , 27th Oct , 2015

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC imetangaza matokeo ya awali katika majimbo 25 ya uchaguzi Tanzania bara na Zanzibar yakiwemo majimbo ya Kibaha, Bumbuli, Jimbo la kusini pemba na Katavi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva atangaza matokeo ya awali ya Urais

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Damiani Lubuva alitangaza matokeo hayo kwa awamu tatu huku akisema leo wataendelea kutangaza majimbo mengine zaidi kadhri matokeo yatakavyowafikia.

Hata hivyo Jaji Damian Lubuva amewatahadharisha wananchi kwa mujibu wa katiba tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka pekee ya kutangaza matokeo ya nafasi ya urais na hivyo kuwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka pale tume itakapokamilisha ukusanyaji wa matokeo yote.

Tume hiyo inatarajiwa kutangaza matokeo ya Urais tena leo kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea kwa mujibu wa Jaji Lubuva.