Kamanda ya Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema Askofu huyo aliaga familia yake na kuelekea wilayani Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya shilingi milioni 2 na laki 5 baada ya kuuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT Sengerema na hata hivyo hakuweza kulipwa fedha hizo na wanunuzi walimtaka aende na nyaraka za umiliki baada ya hapo hakurudi nyumbani
Kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa tukio hilobado unaendelea