Jumapili , 5th Dec , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu leo Desemba 5, 2021 amefungua barabara ya Bagamoyo kipande cha Morocco - Mwenge ambacho ujenzi wake umekamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu

Katika uzinduzi huo Rais Samia amesema ujenzi wa barabara hiyo, ulianza chini ya Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli na angetamani leo aone matunda ya jitihada zake lakini hayupo hivyo watanzania wamuombee pumziko la amani.

Aidha mapema kabla ya Rais Samia kuzungumza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame M. Mbarawa alieleza kuwa upanuzi wa barabara hiyo ya Morroco - Mwenge yenye urefu wa Kilometa 4.3 umefanywa kwa fedha za msaada kutoka Japan jumla ya shilingi bilioni  71.85 za kitanzania.

Zaidi tazama Video hapo chini