Jumatatu , 25th Apr , 2016

Wananchi wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro,wameitikia wito katika kuchangia miradi ya maendeleo iliypitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu baada ya kuchangia zaidi ya shilingi milioni 110.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. George Jackson Mbijima, akimkabidhi Mwenge huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe.

Mradi iliyopitiwa na Mwenge wilayani humo ni pamoja na ujenzi wa madarasa,maabara, Ujenzi wa wodi ya wanaume,mradi wa Maji, Shamba darasa la Mifugo,na mradi wa vijana wa utengenezaji wa madawati ya shule.

Mradi huo wa madawati unaowashirikisha vijana 15 wa mjini Gairo,uliibuliwa na uongozi wa wilaya kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni jitihada za kukamilisha madawati katika shule zote hadi kufikia june Mwaka huu.

Mkuu wa Kikundi hicho Fabian Lukanyila, amesema hadi sasa kikundi hicho kina jumla ya shilingi milioni 39, ambazo ni mchango wa serikali kuu,halmashauri, wananchi na wahisani.

Mwenge wa Uhuru umekamilisha mbio zake mkoani Morogoro,baada ya kukimbizwa katika halmshauri zake 6,ambapo Mwenge huo uliwasha Mkoani humo April 18 mwaka huu na utaendelea na mbio zake mkoani Tanga.