Ijumaa , 17th Sep , 2021

Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema, Rose Mrema, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema, akiwa na mke wake Rose Mrema, enzi za uhai wake

Taarifa zimeeleza kuwa Mama Rose Mrema, amefariki dunia jana Septemba 16, 2021, kwamva aliugua ghafla baada ya kupata mshtuko wa moyo na baada ya kupelekwa hospitali madaktari walisema mishipa mitatu ilikuwa imeziba kwa muda mrefu.