Jumanne , 18th Aug , 2015

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)Mkoa Tanga imekamata shehena ya mifuko 200 ya sukari katika wilaya ya muheza eneo la Mpapayu mkoani Tanga iliyokua ikitokea nchini Brazil kupitia visiwa vya Zanzibar na kupitishiwa katika bandari ya Kigombe

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)Mkoa Tanga imekamata shehena ya mifuko 200 ya sukari katika wilaya ya muheza eneo la Mpapayu mkoani Tanga

Akizungumza kituo hiki meneja msaidizi mamlaka ya mapato mkoa wa Tanga upande wa forodha Bw, Pius Kibahila amesema katika eneo la Kigombe limekuwa maarufu kwa upakuliwaji wa bidhaa nyingi kwa sasa kupitia njia isiyo rasmi.

Bw, Kibahila ameongeza kuwa kumekuwa na mbinu nyingi za upakuaji na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali zinazoingia kinyemela katika eneo la kigombe hali inayopelekea eneo hilo kuwa hatarishi na kuifanya mamlaka hiyo kufanya upelelezi wa kimya kimya ili kuweza kuwabaini wahusika hao.

Aidha ametoa wito kwa waingiza bidhaa nyingi kwa njia ya magendo kuacha mara moja tabia hiyo kwani endapo watakamatwa watanyang'anywa bidhaa zao pamoja na usafiri watakao kuwa wakitumia kupakulia magendo hayo.

Sanjari na hayo amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya aina hiyo katika kipindi hiki hususani uingizwaji wa sukari na mpaka sasa wamefanikiwa kukamata boti mbili za majini ambazo tayari zimeshataifishwa kwaajili ya kufanyiwa mnada.