Alhamisi , 20th Jan , 2022

Alizaliwa  Novemba 23, 1976 katika Kata ya Bulyaga, Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Dkt. Tulia Ackson

Dkt. Tulia alisoma elimu yake ya msingi na sekondari mkoani Mbeya na baadaye mwaka 1998-2003 alisoma sheria  Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mwaka 2005-2007 Dkt. Tulia alifanikiwa kusoma Shahada Ya Uzamivu Huko Cape Town, Afrika Kusini, na  

Baadaye alirudi Dar es Salaam na kuwa mkufunzi wa  Sheria Chuo Kikuu hadi Mwaka 2014 alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Mwaka 2015 alikuwa kati ya wabunge 10 walioteuliwa na Rais kuingia bungeni, na baadaye mwansheria huyu alichaguliwa kuwa naibu spika wa bunge la Tanzania mwaka 2015 hadi hii leo.

Baada ya Januari 6,2022, aliyekuwa spika wa bunge Job Ndugai kujiuzulu, chama cha mapinduzi CCM kilitangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa kumtafuta spika mpya, mchakato ulioanza Januari 11- 15, 2022.

Taarifa ziliripoti kuwa watu 71 walijitokeza kuchukua fomu hizi za kuwania kiti cha uspika ikiwa pamoja na Dkt. Tulia Ackson, ambapo huu leo baada ya kamati kuu ya Halmashauri kuu kufanya kikao Jijini Dodoma wamemteua Dkt. Tulia Ackson kama mgombea wao kwenye nafasi hiyo.

Dkt. Tulia Ackson atatakiwa kujiuzulu unaibu spika wa bunge, jambo ambali litafungua lango la kuanza  kwa mchakato wa kumtafuta Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.