Jumapili , 19th Sep , 2021

Mbunge wa Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma Mhe. Vita Kawawa, amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali.

Picha ya gari kwenye eneo la ajali

Gari hilo limepinduka mara tatu katika kijiji cha Lipepo mkoani Ruvuma walipokuwa kwenye msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Tanzania Bara, Bi. Christina Mndeme.

Kwenye gari hiyo alikuwepo mbunge Vita Kawawa, dereva wake na wasaidizi wake wawili ambao wote wamenusurika.