Alhamisi , 21st Jan , 2021

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum, (CCM), Martha Umbulla, amefariki dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Bunge la Tanzania marehemu ameaaga duni usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya HCG Mumbai.

Spika wa Bunge Job Ndugai ameeleza kupokea kwa mshutuko taarifa hizo na kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, wabunge pamoja na wananchi wa mkoa wa Manyara kwa msiba huo mzito.

Aidha Ofisi ya bunge ikishirikiana na familia itaratibu mipango ya mazishi na kuendelea kutoa taarifa zitakazo kuwa zikijiri.