Alhamisi , 27th Jul , 2017

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero hiyo kwa kutoa mabomba ya kusambazia maji katika kata ya Matumbulu ndani ya manispaa ya Dodoma  yenye urefu wa Kilomita 1 yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 8.

Mh. Mavunde akikabidhi mabomba kwa wananchi.

Ahadi ya kuondoa kero ya maji, Mh. Mavunde aliitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo ameanza kutimiza huku akiwataka wananchi wake kuwa waangalifu na wasimamizi na miundombinu hiyo.

"Kupitia utaratibu huu wananchi wataepukana na adha ya kutafuta maji kwa umbali mrefu. Viongozi mpo hapa naomba msimamie jambo hili kwa kushirikiana na wananchi ili miundombinu hii ya maji idumu kwa kipindi kirefu. Mtu ambaye ataharibu miundombinu hii ya maji atakuwa anahatarisha maisha yako. Walindeni" Mavunde