"Marehemu alikuwa akidandia Treni"- ACP Abwao

Ijumaa , 20th Nov , 2020

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Galula Luhende (50), mkazi wa Malampaka, wilaya ya Maswa, mkoa wa Simiyu, amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni usiku wa kuamkia leo Novemba 20, 2020.

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao.

Akizungumza hii leo Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao, amesema kuwa Treni hiyo ilikuwa ikitokea jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam na kwamba kabla ya ajali ilisimama Malampaka kupakia abiria.

"Marehemu alikuwa akidandia Treni hiyo iliyokuwa imeanza kuondoka, ndipo alipoteleza na kuanguka na kukanyagwa miguu", amesema ACP Abwao.

Aidha Kamanda Abwao ameongeza kuwa, "Marehemu huyo kabla ya kufariki, alikimbizwa Kituo cha Afya Malampaka na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya wilaya ya Maswa kwa matibabu".