Jumanne , 26th Sep , 2017

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa majini wanaendelea na uchunguzi dhidi ya matukio ya mauaji yanayoendelea kutokea katika baadhi ya maeneno na kisha miili kutupwa kwen

Kamanda Mambosasa ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba matukio hayo yanaonekana kudhamiriwa na watu wanaofanya hivyo kwani miili yote inakutwa imefungwa kamba.

"Jeshi la polisi tunaendelea na ufuatiiaji tukishirikiana na askari wa majini kwa sababu matukio haya yanatokea huko, kama kanda tunaendelea tena kwa uchunguzi wa hali ya juu, na hawa wauaji wanakuwa wanadhamiria kabisa kufanya hivyo. Ni vifo vya mashaka kwa kweli na yote inakutwa imefungwa hii inamaanisha huyo mtu anadhamiria", amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kuzungumzia miili mingine ambayo iliokotwa katika fukwe za pwani ya Msasani, na kusema kwamba miili ile haikujulikana ni kina nani na hakukuwa na mtu alikwenda kuripoti kupotelewa na ndugu yake, hivyo waliikabidhi Manispaa kuizika.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mfululizo ya watu kuuawa na kutupwa baharini, na kisha miili yao kuokotwa ikiwa imefungwa kwenye viroba, ambapo jana miili mitatu imeokotwa huku mwili mmoja ukiwa umefungwa jiwe shingoni.