Majengo yanayolipiwa kodi kukaguliwa mtaa kwa mtaa

Ijumaa , 5th Feb , 2021

Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, amewaagiza watendaji wa mikoa kuwatambua wamiliki wa majengo yanayotakiwa kulipiwa kodi ili wazilipe kama sheria ya ardhi inavyoelekeza.

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo

Waziri Jafo ameyasema hayo hii leo Februari 5, 2021, wakati akiongea na maafisa wakuu wa wilaya, maafisa tarafa na wakurugenzi ambapo ametoa muda wa wiki tatu kwa zoezi hilo kukamilika na fedha zitakazokusanywa zinaingizwa moja kwa moja serikalini.

"Leo Februari 5 hadi tarehe 28, 2021,  wiki hizi zote ziende zikatumike kwa ajili ya kwenda kubainisha majengo yote yaliyokuwa katika kila mtaa, tunataka tupate rekodi ya majengo yote ndani ya Tanzania ambayo yanakidhi kulipiwa kodi ya majengo kwa mujibu wa sheria", amesema Waziri Jafo.

Baadhi ya watendaji wamesema katika zoezi hilo watazingatia miongozo ya serikali inavyoelekeza kuhusu ukusanyaji mapato ya serikali.