Jumapili , 19th Sep , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Kagera wahakikishe wanasimia vizuri miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ukiwemo na huo wa ujenzi wa kituo cha maegesho ya magari makubwa Nyakanazi wilayani Biharamulo.

Majaliwa ameyasema jana Jumamosi, Septemba 18, 2021 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Nyakanazi baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho ambao unagharimu sh. bilioni 2.6 na unatarajiwa kukamilika Novemba, 2021.
 

Tazama Video hapo chini