Alhamisi , 9th Jun , 2016

Madiwani 24 wa Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru,jana wamepanda kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi Arusha, kujibu shitaka la kuharibu uzio wa Itandumi Naftani Makere.

Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru,

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Vitalis Timoni, mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Augustine Rwizile, amesema wastakiwa hao kwa pamoja wanashitakiwa kwa kuharibu uzio Mei 4 mwaka huu, huko Leganga Wilaya ya Meru.

Ameendelea kusoma hati hiyo kuwa washitakiw ahao walisababisha hasara ya Sh. Milioni 7 kwa kuharibu uzio huo.

Amewataja washitakiwa hao ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Meru Willy Njau (Chadema), Makamu Mwenyekiti wa halamshauri hiyo, Nelson William, Elisa Stephen, Digna John, Dina Erick, Wilson Fanuel,Josephine Anael, Samuel Ismail, Agness Eliya, Isack Afitwe na Neema Isack.

Wengine ni Gadiel Stanley, Jeremiah Masawe, Peter Efatha, Benard Wilson, Henry Benjamin, Emanuel Pendael, Fadhila Joseph, Penzila Palangyo, Mary Antony, Roman Laurance, Bryson Mosses, Franck Ngoye na Eveline Julius.

Washitakiwa hao ambao wanatetewa na Wakili Charles Abrahamu, baada ya kusomewa hati ya mashitaka, wamekana na wapo nje kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja na mdhamini mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 28 mwaka huu itakapotajwa tena kwa kuwa upelelezi haujakamilika.