Ijumaa , 21st Oct , 2016

Nchi zinazoendelea kote duniani zinaweza kuokoa dola bilioni 21 endapo wasichana wote wenye umri wa miaka 10 wataweza kumaliza elimu ya sekondari.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kishumundu wakiimba wimbo wa Tanzania.

Hayo ni matokeo ya utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA katika ripoti yake kuhusu hali ya idadi ya watu duniani mwaka 2016.

Ripoti inaonesha kwamba wasichana wana fursa ndogo ya kumaliza shule kuliko wavulana na wako katika hatari zaidi ya kukabiliwa na ndoa za mapema, za lazima na ajira kwa wato.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Richard Kollodge ambaye ni mhariri wa ripoti hiyo amesema wasichana kumaliza elimu ya sekondari ni muhimu sana.