Jumatatu , 23rd Jun , 2014

Waandishi wa habari na wadau wa habari wapatao 200 wanatarajiwa kukutana hapo kesho katika kongamano la Mwaka la maadili ya Uandishi wa Habari.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari nchini Tanzania MCT Kajubi Mukajanga.

Pamoja na mambo mengine washiriki wa kongamano hilo watatathmini miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo huria wa vyombo vya habari nchini.

Kongamano hilo lilioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania MCT ambalo Kauli Mbiu ni “Kusherehekea Mfumo Huria: Miongo miwili ya kukua kwa Vyombo vya habari Anuwai Tanzania, litafanyika katika eneo la Ujenzi wa makao makuu ya Baraza la Habari (MCT) huko Kimalang'ombe mjini Bagamoyo kuanzia saa tatu asubuhi.

Wataalamu watakaongoza mjadala huo elekezi ni Prof. Penina Mlama, Bw. Ndimara Tegambwage na Bw. Jenerali Ulimwengu.