Jumatatu , 16th Jan , 2017

Kiwanda pekee cha kutengeneza mataruma ya reli na uchimbaji wa kokoto Afrika Mashariki na Kati kilichopo eneo la Kongolo Kwale wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, kinakabiliwa na uchakavu wa mitambo hali ambayo imepunguza kiwango cha uzalishaji kwa 70%

Kiwanda cha mataruma cha Kongolo Mbeya

Kiwanda hicho ambacho ni mali ya TAZARA, kilianzishwa tangu  mwaka 1977, kwa ubia na nchi ya Uchina na tangu kipindi hicho mitambo yake haijabadilishwa wala kufanyiwa ukarabati, licha ya kuwa na umuhimu mkubwa.

Juma  Mizambwa ni Kaimu Meneja wa Kiwanda hicho anafafanua (Sikiliza sauti yake hapa chini)

Kamati ya Bunge inayoshughulikia miundombinu nchini ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Norman Sigalla, imetembelea kiwanda hicho,  na kutoa  mapendekezo yake  kukinusuru kiwanda hicho (Sikiliza sauti za wabunge hapo chini)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Meneja Mkuu wa Tazara kwa  upande wa Tanzania, Fuad Abdallah imedai kuwa shilingi bilioni 3.5 zinahitajika kununulia mitambo mipya au bilioni 2.2 kufanya ukarabati. (Sikiliza sauti hapa chini)

Nao baadhi ya wadau waliotembelea kiwanda hicho ambao ni wabunge akiwemo Zubery Mchauka na Anna Lupembe wametoa maoni yao (Sikiliza sauti hapa chini)

Sauti ya Juma Mzimbabwe, Kaimu Meneja wa Kiwanda hicho
Sauti ya Mwenyekiti wa kamati Prof. Norman Sigalla
Sauti ya Meneja Mkuu wa Tazara kwa  upande wa Tanzania, Fuad Abdallah
Wabunge Zubery Mchauka na Anna Lupembe