Jumanne , 7th Jun , 2016

Ugonjwa wa Kipindupindu umeigharimu Serikali zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa kuhudumia wagonjwa katika miezi tisa tangu ulipozuka Agosti 15 mwaka jana.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu,

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Dodoma, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, ugonjwa huo umedumu katika mikoa 23 kwa kipindi cha miezi tisa sasa.

Mhe. Ummy amesema kwa Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni mia tisa (900,000,000) mwezi Novemba 2015 ambapo fedha hizo ziligawanywa katika Mikoa iliyoathirika.

Aidha, kiasi kingine cha shilingi 520,000,000.00/= kilitumika Mikoani, shillingi 251,188,940.00/= Dawa na Vitendanishi na shilingi 328,811,060.00/= kwa Kamati za Afya Kitaifa (Subcommittees) mbalimbali kutekeleza shughuli za uelimishaji jamii, mafunzo kwa wataalamu wa afya na vilevile kupeleka timu za wataalamu katika Mikoa ili kutekeleza kazi za udhibiti wa mlipuko.

Kuhusiana na hali ya ugonjwa huo unavyokwenda amesema kuwa Takwimu zinaonyesha kuwa kuendelea kupungua kwa ugonjwa huo kwa mwezi mei ambapo mwezi March kulikua na wagonjwa 2653,April wagonjwa 1024 na mwezi ni wagonjwa 524 tu.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa tangu kutokea kwa ugonjwa huo mwaka jana watu 21634 waliugua ugonjwa huo na 338 kati yao walipoteza maisha kutokana na kukosa matibabu ya haraka.