Jumatano , 10th Feb , 2016

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amemshurukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa mkuu wa chuo na kuahidi kuendeleza upanuzi na uboreshaji wa chuo hicho.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akimkabidhi Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete cheti cha Shahada ya Heshima ya Uzamivu

Akizungumza na viongozi mbalimbali chuoni hapo baada ya kufanya ziara Dkt. Kikwete amesema atahakikisha chuo kikuu cha Dar es salaam kinaendelea kuandaa wataalamu na viongozi na viongozi wa fani mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Dkt Kikwete alitembela vitivo mbalimbali katika chuo hicho kwa ajili ya tafiti na maktaba zitakazowezesha chuo hicho kupokea wanafunzi wengi zaidi ambapo kwa sasa chuo hicho kinapokea wanafunzi 22,000.

Rais mstaafu Kikwete amesema anatamani chuo hicho kiwe chuo kikubwa nchini na Afrika kinachotoa viongozi ambapo mtu akitaka mtaalam yoyote aweze kufikiria kwanza mhitimu wa chuo kikuu kabla ya kufikiria kwingine.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. Rwekaza Mukandala amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Dkt. Kikwete kuwa mkuu wa chuo hicho kutokana na mchango wake katika chuo wakati yupo madarakani.