Kauli ya Vicky Kamata baada ya mume wake kufariki

Jumamosi , 20th Feb , 2021

Aliyewahi kuwa mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata, ameandika kuwa alidhani yeye ni jasiri, baada ya kumpoteza mume wake Dkt.Servacius Likwelile, aliyefariki dunia hii leo baada ya kuugua ghafla

Vicky Kamata, akiwa na mume wake Dkt.Servacius Likwelile, wakati wa uhai wake

Vicky Kamata, ameyaandika hayo hii leo Februari 20, 2021, kupitia akunti yake ya mtandao wa Instagram.

"Nilidhani mimi ni jasiri, lakini kwa hili kumbe mimi si lolote, Mungu mbona umeniacha?", ameandika Vicky Kamata

Dkt. Servacius Beda Likwelile, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na pia aliwahi kuwa Mhadhiri Idara ya Uchumi na Ndaki ya Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.