Jumanne , 12th Jul , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli amewataka wakurugenzi aliowateua kwenda kusimamia fedha za serikali pamoja na kuondoa kero za Wananchi zinazowazunguka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.

Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa kiapo cha Maadili kwa wakurugenzi wa wilaya 185 nchini, rais Magufuli amesema kuwa ametumia muda mrefu kuwafatilia kuwateua wakurugenzi hao ili waweze kusimami ipasavyo sera za serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo.

Rais Magufuli amesema kumekuwepo na matukio ya ubadhirifu wa fedha za serikali kwa baadhi ya wakurugenzi waliopita hivyo amewataka kwa wakurugenzi walioteuliwa kuwatumikia wananchi na kuepuka matumizi mabaya ya fedha za Umma.

Mhe Rais amesema kuwa wakurugenzi hao watambue kuwa kuna majaribu mengi katika Halmashauri wanazoziongoza ikiwemo kurubuniwa na wafanyabishara katika uingiaji wa mitakaba mbalimbali ambayo mingi inakua na Maslahi binafsi.

Mhe. Magufuli amesema kudhihirishia hilo ndio maana kati ya Wakurugenzi 185 waliopita ni 60 ndio wamefanikiwa kurudishwa kwenyer jopo la sasa na kuongeza kuwa ana imani kubwa na utendaji kazi ya wa wakuregenzi wapya aliowateua.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli