Ijumaa , 16th Mei , 2014

Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt Titus kamani amewata wananchi wa mikoa ya kaskazini kuwafichua wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za mifugo na vyakula kwa njia za panya kutokna nje ya Tanzania.

Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt Titus kamani

Wananchi   wanaojishughulisha  na  ufugaji  wa  kuku  katika  mikoa ya  kanda  ya kaskazini   wamelalamikia   uingizaji   wa  vifaranga  na kuku  wa  nyama   kutoka  nje  ya  nchi.

Wafugaji hao wakitoa kilio chao kwa Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt Titus kamani, wamedai  kuwa   licha   ya  tatizo hilo kuwaathiri   kiuchumi  linaweza kuhatarisha  afya  za  walaji .

Wajasiriamali  hao wametoa malalamiko yao    kwa   waziri   wa  mifugo   Dkt  Titus  Kamani  aliyetembelea  baadhi   ya   miradi ya wananchi  hao  wilayani  Arumeru  mkoani  Arusha .

Akizungumzia tatizo hilo  waziri Kamani  amewaomba  wananchi  kusaidiana  na  serikali  kuwafichua  watu hao   kwani wanachofanya ni  uhalifu   na  pia  amewataka  kuendelea kuelimisha  jamii    madhara   ya   matumizi  ya bidhaa  zinazoingizwa kwa  njia  za  panya.

Uingizaji   wa  bidhaa  kwa  njia  za  panya ni miongoni   mwa  changamoto   kubwa   zinazoikabili   mikoa   ya   kanda   ya   Kaskazini kutokana  na kuwa  na  njia  nyingi  za  panya ambazo   pia  zimekuwa   zikitumika   kuvusha   bidhaa   na   vyakula   kwenda  nchi.