Jumatano , 15th Feb , 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema anataka kupiga vita tabia ya ushoga kwani anadai wanaofanya hivyo wanajiendekeza, huku akiweza wazi mtindo atakaotumia kuwakamata

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla

Kigwangalla amesema kwa kuanza vita hiyo ya kupambana na ushoga Tanzania, watataja majina ya mashoga wote wanaofanya biashara hiyo kupitia njia za mtandao kisha hao mashoga ambao watakuwa wamethibitika kujihusisha na tabia hiyo wataisaidia serikali kuwapata wenzao. 

"Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ushoga unaendelea. Watakamatwa kimya kimya! serikali ina mkono mrefu. Wakipatikana watatusaidia wenza wao, kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na tutaishinda. Mtandao ni mrefu na nitaendesha operation kamata kamata, watu wakumbuke kuwa ushoga hauna addiction wala siyo wa kuzaliwa nao, wanaofanya hivyo wanajiendekeza tu! Ushoga siyo biological. Mashoga wote waache mara moja" alisisitiza Dkt. Hamisi Kigwangalla

Naibu Waziri wa Afya,  Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye sasa yupo ziarani kikazi katika jimbo lake la Nzega mkoani Tabora, anadai akimaliza ziara hiyo akisha rudi Dar es Salaam kabla hata ya kuhamia Dodoma atataja orodha kamili ya mashoga wanaojiuza mitandaoni.