Jeshi la polisi latoa taarifa

Monday , 13th Nov , 2017

Jeshi la Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam limetoa taarifa rasmi juu ya ajali ya moto iliyoteketeza nyumba ambayo ni makazi ya watu katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam.

Akiongea na mwandishi wa East Africa Television Kamanda wa Polisi Msaidizi Kanda Maalum Benedict Kitalika, amesema moto huo amabo ulitokea leo majira ya saa 3 asubuhi, haujajulikana umesababishwa na nini lakini umeteketeza mali zote zilizomo kwenye nyumba hiyo, ambazo pia thamani yake bado haijajulikana.

Kamanda Kitalika amesema moto huo ambao ulianza katika chumba kimoja anachoishi mpangaji na kisha kusambaa kwenye vyumba vingine na kuteketeza nyumba yote, haujaleta madhara kwa binadamu kwa kutokuwa na taarifa yoyote ya kifo au majeruhi.

 

 

Nyumba ambayo imeteketezwa kwa moto leo asubuhi