Jumapili , 18th Apr , 2021

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo ameeleza kusikitishwa kwake na vijana 854 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamekiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kufanya maandamano ya kwenda Ikulu kutaka kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo

Akiongea wakati wa hafla ya kutunukiwa Shahada Maafisa wapya wa JWTZ waliohitimu kozi ya 1 ya Shahada ya 1 ya Sayansi ya Kijeshi Jenerali Mabeyo amesema vijana hao walitaka kuandamana kwenda Ikulu kumuona Mhe. Rais Samia Suluhu, ili wadai kuandikishwa Jeshini kama walivyoahidiwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

'''Vijana hao ni kati ya vijana 2,400 walioahidiwa kuandikishwa Jeshini na walifanya uamuzi huo baada ya Jeshi kuamua kuwapunguza katika kazi ya ujenzi wa Ikulu Chamwino baada ya kazi kupungua ili waende kufanya katika kazi maeneo mengine, lakini wao wakapinga kwa madai wangekosa kuandikishwa Jeshini,'' amesema.

Zaidi tazama video hapo chini