Jumatano , 10th Jun , 2015

Serikali ya Japani yasaini kuisaidia Tanzania dola za kimarekani milion 38 kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya umeme.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la umeme nchini Tanzania TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba amesema shirika hilo litamaliza tatizo la umeme nchini na hasa jijini Dar es salaam la kukatika umeme mara kwa mara.

Mhandisi Mramba ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa kuimarisha sekta hiyo ya umeme nchini kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Japan.

Mramba amesema mradi huo ni msaada kutoka serikali ya Japan umekuja nchini kwa muda muafaka kutokana na hali iliyopo ya uchakavu mkubwa kwenye baadhi ya miundombinu ya zamani ambayo inatumika hadi leo kwenye kuzalisha umeme na pia za kuongezeka kwa presha ya huitaji wa huduma hiyo nchini