Jumatano , 20th Oct , 2021

Jaji Kiongozi Mustapha Siyani, aliyekuwa akisikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake, amejitoa kusikiliza kesi hiyo.

Jaji Kiongozi Mustapha Siyani, aliyejitoa kusikiliza kesi ya Mbowe na wenzake

Jaji Siyani amejitoa hii leo na kusema kwamba amechukua maamuzi hayo kwani hataweza kusikiliza shauri hilo mfululizo kutokana na majukumu yake mapya ya Jaji Kiongozi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kumaliza kutoa uamuzi wa shauri dogo kwa kutupilia mbali mapingamizi mawili ya utetezi katika kesi ndogo ya Freeman Mbowe na wenzake, la kutaka maelezo ya Adamu Kasekwa yasipokelewe kwa madai yaliwasilishwa nje ya muda wa kisheria na mtuhumiwa alitishiwa kuteswa.