Alhamisi , 14th Mar , 2024

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP Camillus Wambura

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Kamanda Mkoa wa Songwe SACP Theopista Mallya amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Tanzania inaeleza kuwa SACP Mallya anakwenda kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Martin Otieno aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.