Jumamosi , 18th Apr , 2015

Baraza la Habari nchini Tanzania MCT limesema idadi ya wateule katika tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania EJAT kwa mwaka 2014 imepungua ikilinganishwa na mwaka jana.

Katibu mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, katibu mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga amesema tuzo hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa wanahabari waliofanya vyema katika kazi zao na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamedi Gharib Bilal April 24 mwaka huu.

Kajubu amesema kati ya wateule 53 xwaliteuliwa na jpo la majaji 43 wanatoka kwenye magazeti ambapo imepungua kwa wateule 12 ililinganisha na tuzo za mwaka 2013.

Aidha Kajubi ameongeza kuwa kwa upande wa radio ni 17 pia ikionekana wateule kupungua kwa 22 ikilinganishwa na mwaka jana huku upande wa runinga idadi ya wateule ikipungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na wateule wawili tu.

Hii itakuwa ni mara ya sita kuwatunza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi katika mwaka uliotangulia ambapo katika tuzo hizo makundi mbalimbali kumi na tisa ndio yatakayopewa tuzo hizo.