Huduma ya LUKU kukosekana kwa saa 12

Friday , 17th Mar , 2017

Watumiaji wa umeme nchini watakosa huduma ya ununuzi wa nishati hiyo kwa njia ya LUKU kwa takriban saa 12, kutokana na kuzimwa kwa mfumo unaohusika na huduma hiyo.

Taarifa iliyotolea na Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) imesema kuwa mfumo huo utazimwa kuanzia siku ya Jumapili Machi 19 saa 4 usiku hadi siku ya Jumatatu saa 3 Asubuhi.

“Lengo ni kuboresha Mfumu wa LUKU katika uhifadhi wa wateja (Database). Tunaamini maboresho haya yatasaidia ufanisi katika manunuzi ya umeme” Imesema taarifa hiyo iliyotolewa leo na kitengo cha mahusiano cha TANESCO.

Aidha, shirika hilo limewataka watumiaji kufanya manunuzi kabla ya saa 4 usiku siku ya Jumapili na kuomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Recent Posts

Msanii Beka Flavour

Entertainment
"Simuogopi wala simfikirii Aslay" - Beka Flavour

Matajili wa Alizeti timu ya soka ya Singida United ya Singida wakijifua jijini Mwanza.

Sport
Singida United yasajili 16

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Current Affairs
Tiba asili na tiba mbadala wabanwa

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Current Affairs
Wabunge nane CUF wavuliwa Uanachama