Jumapili , 17th Jan , 2021

Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa gharama za bilioni 3.9 imeanza  kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akizungumza jambo na manesi wanaofanya kazi katika hospitali ya Uhuru iliyopo Wilayaya Chamwino Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Dkt.Eusebius Kessy alipokuwa akiongea  na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.

Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa Dkt.Kessy amesema kwa sasa huduma za maabara,clinic za macho na meno,mionzi ,clinic za mama na mtoto na huduma za wagonjwa wa nje (OPD).

Hospitali yetu imeanza kutoa huduma tangia tarehe 21 Desemba 2020 na mpaka sasa imeshahudumia wateja takribani 300”amesema Dkt. Kessy.
   
 Kwa upande wake Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe ambae alifanya ziara maalum kukagua imaendeleo ya Hospitali hiyo amesema kuwa kuwa ujenzi wa hospitali iyo umekamilika kwa asilimia 99.8.

Amebainisha kuwa maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu alipofanya ziara Novemba 20,2020 yametekelezwa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo, miundombinu muhimu na ukamilishaji wa ukuta kuzunguka hospitali hiyo ambao umekamilika kwa asilimia 99 na ujenzi wa miundombinu ya barabara hospitalini hapo unaendelea chini ya TARURA na utakamilika hivi karibuni.