Jumanne , 26th Oct , 2021

Msanii wa bongo fleva na balozi wa Mazingira, Ben Pol, amesema kuwa katika hifadhi zote nchini, anapendelea zaidi kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuwa ina eneo kubwa na mandhari tofauti.

Ben Pol

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 26, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio na kusema kwamba katika nafasi yake ya ubalozi aliyoteuliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, ni ya kusimamia udhibiti wa taka ngumu.

"Kivutio changu pendwa cha utalii ni Serengeti sababu ina scenaries tofauti tofauti nyingi, unaweza ukawa Serengeti ukajiona upo Manyara, mandhari tofauti na ina idadi kubwa sana ya wanyama ikilinganishwa na mbuga zingine," amesema Ben Pol