Jumanne , 30th Jun , 2015

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imesema kumekuwa na kiwango kikubwa cha ukiukwaji wa haki ya kuwapa chakula watoto wanaotumikia vifungo magerezaji pamoja na wenye umri chini ya miaka mitano.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Bahame Nyanduga

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Afisa Dawati la Watoto wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Fides Shao amesema watoto walio magerezani wanachanganywa na wakubwa na pamoja na Ttizo la Ukeketaji watoto Wachanga.

Aidha Bi. Fides amesema kuwa unyanyasaji mwingine dhidi ya watoto ni kuwa bado kuna shule zinatekeleza adhabu ya viboko lakini pia kwa upande wa jamii za wafugaji kutokana na kuhama kutafuta malisho ya mifugo watoto wengi wanakosa elimu ambayo ni haki yao ya msingi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ua Afya na Ustawi wa Jamii katika kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto, Uniti ya Jinsia na Haki za Binadamu, Bi. Notgera Ngaponda amesema wizara imekuwa ikitoa elimu kwa wahudumu wa afya ili kuondokana na unyanyasaji kwa watoto.