Alhamisi , 16th Sep , 2021

Idadi ya mahabusu ambao ni raia wa Ethiopia katika Gereza la Maweni mkoani Tanga imefikia 496 idadi ambayo ni inazidi idadi ya mahabusu ambao ni raia wa Tanzania ambapo serikali imesema iko mbioni kutatua idadi hiyo kwani imepelekea magereza kuelemewa na mzigo wa kuwalisha raia hao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo, baada ya kutembelea Gereza la Maweni mkoani Tanga ambapo pia alitembelea mpaka wa Horohoro,uliopo wilayani Mkinga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya.

Akitaja makusanyo ya serikali katika kituo cha forodha kilichopo katika mpaka wa Horohoro, Afisa Mfawidhi Forodha, Mohamed Shmate, amesema wamekusanya hadi kuvuka lengo kwa kufikia asilimia Mia Moja na Ishirini na Tano ndani ya miezi miwili.