Jumatatu , 6th Jun , 2016

Chama cha wananchi CUF nchini Tanzania kimeitaka serikali kupitia jeshi la polisi kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya kinyama visiendelee kutokea ikiwemo vya mauji ya wananchi wasio na hatia kama vilivyotokea mkoani Tanga hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama cha CUF, Shaweji Mketo

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama cha CUF, Shaweji Mketo amesema kuwa serikali lazima ibaini chanzo cha mauaji hayo na kuchukua hatia za haraka kwa wahusika wa matukio kama hayo.

Katika hatua nyingine Shaweje amesema kuwa katika kujiimiarisha zaidi kwa Chama hicho kimetangaza kufanya mkutano mkuu wake wa taifa ili kujaza nafasi zilizo wazi za uongozi kuweza kukiimarisha ambapo nafasi zinazotarajiwa kujazwa ni pamoja na ile ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.

Shaweji amesema kuwa Chama hicho kimebaini kuwa Watanzania wengi wamekata tamaa na hali ya maisha inayoendelea sasa hivyo kupitia kujiimarisha kwa chama hicho wataweza kufanya mageuzi chanya katika maendeleo ya taifa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama cha CUF, Shaweji Mketo