Jumanne , 18th Nov , 2014

Tume ya Usuhishi (CMA) inataraji kutoa maamuzi wakati wowote kuhusiana na kesi za watumishi watatu waliofukuzwa kazi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kubainika kuwa walijihusisha na udanganyifu bandarini.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchni imefanya ukaguzi wa baadhi ya mizigo iliyotiliwa shaka na kubaini katika makontena 270 kati ya 546 yaliyokaguliwa katika ya mwezi Aprili na Juni yalikutwa na makosa mbalimbali.

Akijibu swali la mbunge wa Konde Mhe. Khatibu Haji aliyetaka kujua ni wafanyakazi wangapi wa TRA walibainika kujihusisha na hujuma kutokana udanganyifu uliokuwa ukifanywa na mawakala wa uondoaji wa mizigo Bandarini wakishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchni-TRA.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema uhakiki huo ulibaini jumla ya wafanyakazi Tisa waliohusika na udanganyifu huo wa kuandika taarifa ambazo siyo sahihi juu ya mali zilizokuwemo ndani ya baadhi ya makontena ambapo mamlaka ya nidhamu ilichukua hatua ya kuwaondoa kazini watumishi watano na wanne waliobaki walikutwa hawana hatia.

Amesema kati ya watu hao watano walioondolewa kazini, watumishi watatu wamekataa rufa tume ya usuluhishi na usimamizi-CMA na mtumishi mmoja amekata rufaa kwa kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato.

Aidha maamuzi ya mwisho yatategemea uamuzi wa CMA na kamishna mkuu.