Ijumaa , 17th Nov , 2017

Mahakama ya Juu nchini Cambodia imekifuta chama kikuu cha upinzani nchini humo CNRP (Cambodia National Rescue Party), na hivyo kumpa nafasi Waziri Mkuu Hun Sen kuendelea kusalia madarakani.

Chama cha CNRP, ambacho kimekua na matumaini ya kumuangusha Waziri Mkuu, madarakani kwa zaidi ya miaka thelathini, wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, kinashutumiwa kula njama za kuipindua serikali, shutma ambazo chama hicho kimezikanusha

Wachambuzi wanaona uamuzi huo wa mahakama ni shinikizo kutoka kwa chama cha tawala dhidi ya upinzani, vyama vya kiraia na vyombo binafsi vya habari ili kunyamazisha upinzani wotewote wakati wa uchaguzi wa mwaka 2018 .

Kiongozi wa chama cha CNRP, Kem Sokha, alikamatwa tarehe 3 Septemba akishtumiwa kujaribu kupindua serikali ya zamani ya Khmer Rouge kwa ushirikiano na Marekani.

Mahakama pia imewapiga marufuku wanasiasa 118 wa upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa kipindi cha miaka mitano.