Jumanne , 3rd Mar , 2015

Serikali imesema ipo mbioni kupeleka Bungeni mpango wa tatu wa Taifa wa kupambana na rushwa ambao utajumuisha taasisi mbalimbali za Umma Ikiwa ni mkakati madhubuti utakaosaidia kuondoa vitendo vya utoaji na upokeaji wa Rushwa Nchini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utawala bora Kapten Mtaafu Geogre Mkuchika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utawala bora Kapten Mtaafu Geogre Mkuchika amebainisha hayo Jijini Arusha katika Mkutano wa kuandaa mpango wa kupambana na Rushwa ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA uliowajumuisha pia watendaji wa vyombo ya ukusanyaji mapato kutoka katika nchi za Afrika Mashariki

Waziri Mkuchika amesema Tanzania imekuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na rushwa kwenye vyombo vyake vya ukusanyaji mapato ambapo licha ya uwasilishwaji bungeni wa mpango wa taifa wa kupambana na rushwa pia sheria ya manunuzi PPRA nayo ipo mbioni kufanyiwa marekebisho ili iweze kuleta tija kwa taifa..

Awali Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Rished Bade amesema TRA ni miongoni mwa vyombo vilivyopo katika mazingira hatarishi ya Rushwa na hivyo kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kupambana na hali hiyo ikiwemo njia ya kuwakutanisha wadau wakiwemo watu kutoka sekta binafsi na taasisi za dini.

Kwa mujibu wa TRA inayohusika katika mfumo wa makusanyo wa kodi,Mpango wa tatu wa taifa wa wa kupambana na rushw pia inaangalia uwezekano wa kujumuisha ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo vidogovidogo zikiwemo halmashauri ili kuweka mfumo mmoja utakaosaidia kumpunguzia adha mwananchi mlipakodi.