Jumapili , 17th Sep , 2017

Watoto watatu waliokuwa wakichunga ng'ombe katika Kijiji cha Nafco  kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli mkoani Arusha wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu walilolichezea wakidhani ni mpira.

Tukio hilo linadaiwa kutokea  Ijumaa jioni ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Julius Mhale amesema watoto hao wanatarajiwa kuzikwa Jumatatu Septemba 18 

Mwenyekiti huyo amesema kuwa eneo ambalo bomu lililipuka hutumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mazoezi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi hapo baadae.